Likizo ya Aprili

Likizo ya Aprili, nimo njiani ningoje,
Kidato cha kwanza nili, ya kwanza livu ‘ngoje,
Ubozi na ukabili, kunipotosha usije,
Likizo ya Aprili, sinijie kwa ukali.

Likizo ya Aprili, nimo njiani ningoje,
Kidato nimo cha pili, ya nne livu ningoje,
Mabaya tayakabili, kuniharibu yasije,
Vitabu nitavisoma, sitapoteza wakati.

Likizo ya Aprili, nimo njiani ningoje,
Kidato cha tatu nili, kwa ubaya usije,
Vya upuzi kamwe sili, kunipotosha visije,
Mabadiliko tafanya, ubozi niumalize.

Likizo ya Aprili, nimo njiani ningoje,
Kidato cha nne nili, kwa umakinifu nije,
Wakati wanikabili, nao mtihani uje,
Takuwa mmakinifu, muda sitaupoteza.

© Samuel Nguru Mwangi

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Baruapepe yako haitaoneshwa hadharani. Maeneo yenye alama * ni lazima yajazwe!