Furaha Ndani ya Yesu

Nalitunga shairi hili,kwa furaha na bashasha,
Maneno siyo mawili,mengi ndugu nawapasha,
Tushukuru mola kweli, hapa ametufikisha,
Liberia huko mbali, kanisa tulianzisha,
Malawi tuliwasili, ya Mola twawapasha.

Kumi miaka takribani, mengi twasherehekea
Mungu si adhumani, baraka ametushushia
Twafunzwa kwa makini, ukweli tuagundua
Tumeishi ugandani, yote hiyo miakaa
Watumishi twawamini, kufundisha bibilia.

Rabuna yote mpaji, chochote hana shetani
Mbinguni tunataraji, juu ya yetu imani
Siku ya kiama jaji, huenzi huko mbinguni
Rabuna tawafariji, wale wanaomwamini
Mungu tatuvisha taji, twafunza haya chuoni.

Ni muhimu shangilia, mola ametujalia
Watumishi wako pia, yeye wamutumikia
Kwake tunafurahia,hatuenzi ya dunia
Yesu ametupokea, ndani yake furahia.

© Maja Waithaka

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Baruapepe yako haitaoneshwa hadharani. Maeneo yenye alama * ni lazima yajazwe!