Uzuri wa Mkakasi

Lipokuona ukipita, kwa hamu nilikuita
Kakuita jina rita, ila ukazidi kupita
Jina langu ukinita, kuitika sitasita
Hakika wametata, mwachoni mwangu we nyota.

Loi hii ya wahedi, najipata mebung’aa
Ukweli nakuahidi,hisia lisisimuaz
Ilikuwa siku ya Idi, umati linitania
Nikajiekea ahadi, majaliwa takuoa.

Sikupoteza muda, kutayarisha ndoani
Ulio mchache muda, kajipata harusini
Ridhi la maua shada, yonyesha tumeoani
Tuna ta muhimu mada, yakuishi pamojani

Tuliona kwa kasi,nikamini wanipende
Lizingatia ukwasi,likua na nia pinde
Linitia wasiwasi,likosa wangu upande
Uzuri wa mkakasi, ndani cha mti kipande

Wangwana walinitania, wanena nina kiraka
Nimeshindwa vumilia, nakukabidhi talaka
Utatalii dunia, una yako mamulaka
Haraka nilinyakua, zikanihepa baraka.

© Waithaka Ndung’u

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Baruapepe yako haitaoneshwa hadharani. Maeneo yenye alama * ni lazima yajazwe!