Chaguo Maishani

Alitunga kimakini, namini tanichukua,
Nisikize kwa makini, naapa kukuchukua,
Ingawa mi maskini, mahaba nakumwagia.

Nakupenda we kumbuka, naamuka akiwika,
Shuka mi hujifunika, kukicha nacha lishika,
Harusi tutawalika, mkono nitakushika.

Wakumbuka mpenzi, ukweli twatoka mbali,
Hakika nakuenzi, ‘kupenda kwa yangu hali,
Tutaenda kwa wazazi,penzi letu halali.

Usisikize jirani, hakika takupotosha,
Fikiria kwa makini, yote wanayokupasha,
Usije ukajutani, nyumbani moto kiwasha.

Japokuwa sina mali,kitu muhimu kindani,
Ng’amua nastahili, kuwa wako maishani,
Simtafuti wa pili, wanifaaa mileleni.

© Waithaka Ndung’u

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Baruapepe yako haitaoneshwa hadharani. Maeneo yenye alama * ni lazima yajazwe!