Jozi

Halua iwe kwa lozi, na ambari na zinduna,
Jito nalo na matozi, pia jito na kuona,
Nalo neno laazizi, kwao wanaopendana.
Muradi mambo ni jozi, ndipo mambo yakafana.

Ni uzazi na ulezi, mvyele kwa wake mwana,
Mja apigapo mbizi, ni maji ameyaona,
Itoapo tui nazi, na mbuzi imeikuna,
Muradi mambo ni jozi, ndipo mambo yakafana.

Kazi nayo na ujuzi, maarifa kufaana,
Upweke katu huwezi, ni lazima kuungana,
Ibada utegemezi, ni lazima hiyo bwana,
Muradi mambo ni jozi, ndipo mambo yakafana.

©Rashid Mwaguni.

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Baruapepe yako haitaoneshwa hadharani. Maeneo yenye alama * ni lazima yajazwe!