Kiswahili 

Himdi naabtadi, jinale Jala Jalali,
Wa akhiri na wahedi, chanzo cha kila usuli,
Tenapo kisha nirudi, nirudi mara ya pili,
Nisifu lugha ya jadi, lugha yangu Kiswahili,
Tupende lugha faridi, tukipende kiswahili.

Lugha ya tangu jadudi, tangu enzi na azali,
Tuienzini abadi, tukizingatia ngeli,
Tuzishike abjadi, manenoye na methali,
Lugha tusiisharidi, tukatukuza za Mbali,
Tupende lugha faridi, tukipende Kiswahili.

Lugha tuloifanidi, kwa nzuri zake kauli,
Mvuto halwaridi, na utamu wa asali,
Tuzidi kutia chudi, yenee kila mahali,
Kwa zaidi na zaidi, katika zetu shughuli,

Natuifanye fuadi, azizi lugha halili,
Tusome tuwe weledi, Kwa ugwiji na unguli,
Uwe uvumba na udi, kukuza lugha aali.
Nathari iktisadi, zijengwe kitaamuli,

Tupende tuzifaidi, fani zake bulibuli,
Tuwape kama zawadi, wageni wa bara hili,
Kuchunguza tushitadi, kuondoa mushkili,
Marashi ya haliudi, kinukie Kiswahili,

Sheng ni wake hasidi, tumfisheni ni nduli,
Kwepuka tujitahidi, ikiwa tunakijali,
Ughaibu tukinadi, China hata Brazili,
Zile nchi za baridi, kwa ndege reli na meli,

Kikomoni sina budi, kukomea hapa bali,
Tuseme tukijirudi, tukosoane ya kweli,
Naradidi tashdidi, Kipe hadhi Kiswahili,
Takkhmisa ya Rashidi, ya beti nane kamili.

© Bin Mwaguni Rashid.

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Baruapepe yako haitaoneshwa hadharani. Maeneo yenye alama * ni lazima yajazwe!