Wito wa Uhalifu 

Maisha ya siku hizi,  megeuka kiunyonga,
Suala hili la wizi, siku hizi lajijenga,
Kila siku wizi wizi, kweli limekuwa janga,
Huu wito wa uhalifu, si utiliwe makini!

Wezi hawatambuni, bwanyenye ama kabwela,
Wasema wako ’ kazini’, ya kuzitafuta  hela,
Wasomaji tambueni, hawatu wawanyemelea,
Huu wito wa uhalifu, si utiliwe makini!

Mbinu kadhaa wazitumia, kuwahadaa walimwengu,
Kwa imani watazamia, halitavunjika jungu,
Silaha wanazotumia, zaumiza kama rungu,
Huu wito wa uhalifu, si utiliwe makini!

Tujiulize tafadhari, twaweza kuukomesha?
Hebu yatafakari, yatakuwaje maisha?
Maisha bila hatari, uwoga yatakomesha,
Huu wito wa uhalifu, si utiliwe makini!

Kamba tukizikaza, hatua kuzichukua,
Ujumbe kuutangaza, kuhusu kuutatua,
Mswada unaotumeza, takwepa kulipa dia,
Huu wito wa uhalifu, si utiliwe makini!

Kabla ya wino kuisha, maneno nayasheheni,
Lazima wizi uisha, na ukome hadharini,
Kwa hayo nahitimisha, wasomi buriani,
Huu wito wa uhalifu, si utiliwe makini!

© Samwel mwangi Gathia

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Baruapepe yako haitaoneshwa hadharani. Maeneo yenye alama * ni lazima yajazwe!