Viongozi Wapotovu

Nimefi ka mimi leo, kuwapa la tahadhari,
Wazalendo nyi mlio, ndakindaki muwe heri,
Mwepuke nafiki hao, wenye ahadi furi,
Viongozi wapotovu, wakatae chaguzini.

Kote mahali zunguka, uvumi mwingi eneza,
Kampeni moto waka, maneno tamu mejaza,
Wananchi laghaika, hadi bungeni fuliza,
Viongozi wapotovu, wakatae chaguzini.

Wengi zeekea huko, warudishwha kira mara,
Wajidai heshimiko, mamlaka vichwa fura,
Muda mwingi mekuweko, watuona sisi jura,
Viongozi wapotovu, wakatae chaguzini.

Che matusi wayasamba, kama u moto wa nyika,
Wao pinzani sambamba, patana ndoto tendeka,
Maneno chafu waamba, mamlaka twayataka,
Viongozi wapotovu, wakatae chaguzini.

Kujigamba wajigamba, Mola ashatutegua,
Mafanikio wayatamba, na uhondo kitalanta,
Kote beba simutamba, siasa ziwepangika,
Viongozi wapotovu, wakatae chaguzini.

© Samwel mwangi Gathia

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Baruapepe yako haitaoneshwa hadharani. Maeneo yenye alama * ni lazima yajazwe!