Makala

Yafuatayo ni makala mapya  kutoka kwa blogu yetu ya Mwanagenzi Mtafiti. Hapa utayasoma mengi yanayoelimisha na kufahamisha.

Blogu: Mwanagenzi Mtafiti

Mshairi: Moses Chesire

Ushairi ni kipera kimoja cha fasihi ya Kiswahili,dhima ya ushairi sawa na fasihi ya Kiswahili ni kuonya kufunza kuelimisha n.k. hivyo basi washairi wanapozitunga kazi zao walenge kuielimisha jamii na kuifanya iwe bora zaidi. Kwa hivyo ushairi utumiwe kama kioo cha jamii.

Android: Jifunze Ushairi

Je wewe ni mshairi chipukizi ambaye ungependa kuinua tajiriba yako ya utunzi? Je ungependa kujiburudisha kwa maswali ya kusisimua ya chemsha bongo kuhusu ushairi? Ama una azimio la kufanya utafiti kuhusu ushairi wa Kiswahili? Tuna jawabu!

Mshairi: Vincent Okwetso

Vincent Okwetso alizaliwa Butula, Kaunti ya Busia. Ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Masinde Muliro, katika kaunti ya Kakamega anakosomea ualimu. Vincent alianza kutunga mashairi mwaka 2017 mwezi wa kumi tarehe 26, ambapo ilikuwa siku ya marudio ya kupiga kura zilizokuwa zimefanyika mwezi wa nane tarehe nane mwaka 2017. anakumbuka vyema akiwa Nairobi, kura …

Mshairi: Bonface Khaemba Wafula

Uandishi ni kipaji adimu na kama vile kipaji chochote kile huhitaji kupaliliwa na kuchochewa mara kwa mara. Uandishi huchochewa kwa kusoma zaidi na kufanya utafiti zaidi. Ili uzidi kubobea katika uandishi, mazoezi ni kitu muhimu sana. Huwezi kuwa mwandishi kama huandiki, mshairi kama hutungi au mwalimu kama hufundishi. Uandishi ni tunu adhimu na adimu yenye …

(Android) Ushairi wa Mwanagenzi

Ushairi wa Mwanagenzi ni kitumizi cha Android kinachompa tumaini mshairi chipukizi aliye na ari ya kuwa malenga ili kuendeleza fani ya ushairi. Pamoja na kuimarisha washairi chipukizi. kitumizi hiki huelimisha na kuchanganua masuala tofauti yanayohitajika katika ushairi bora. Utasoma mengi kutoka kwa washairi chipukizi nchini Kenya na Tanzania. Makala yametolewa kwa tovuti ya www.mwanagenzi.com iliyo …

Mshairi: Mwangi wa Githinji

Mwangi wa Githinji ni mshairi ambaye amekuwa akiyatunga mashairi kwa miaka mingi. Ni Mwalimu katika shule ya msingi Limuru Township. Amekuwa akitunga mashairi ya sherehe za kifamilia pamoja na sherehe za mahasibu wake. Mashairi yake yameweza kutumika katika tamasha za mziki hadi kiwango cha kitaifa. Mashairi yake huacha wengi wakibung’aa kwa tungo zenye kuelimisha si …

Mshairi: Marko John Kinyafu

Marko John Kinyafu alizaliwa Juni 22 mwaka wa 1995 22 mjini Dar-es-salaam,Tanzania. Ni mtoto wa mwisho kwenye familia ya watoto watatu. Lakabu yake Muumini wa Kweli ndilo jina alitumialo katika kazi zake za sanaa za maigizo ya jukwaani na kazi za ushairi. Marko alianza shule ya awali mwaka 2001. Alisoma kwa miaka miwili na mwaka 2003 alianza …

Ninaweza Kutunga!

Si kwamba ulizaliwa ukiwa bingwa. Ufanisi huja kwa hatua za jitihada. Unaposikiliza watu na kuyaamini, huenda ukafa moyo au ukawa na nguvu na ujasiri wa kuendelea. Leo ningependa kuwatia moyo washairi chipukizi walio na ari ya kutunga ushairi bora. Nilianza kutunga mashairi nikiwa darasa la tano katika shule ya msingi ya Gatei, jimbo la Kiambu. …

Wosia kwa Mwanao

Mwambie mwanao afanye kazi kwa malengo na kujituma kiwango cha salio lake la banki siku moja lifafane na namba zake za simu. Mwambie awe na nidhamu ya pesa na ajenge utamaduni wa kutunza pesa na kuweka akiba. Mwambie aige kutafuta pesa na asiige matumizi. Mwambie aipende pesa kwa vitendo na sio kwa hisia. Kila mtu …

Mshairi: Emmanuel Charo

Mshairi hufurahia anapotunga mashairi yatakayosomwa na watu wengi na bila shaka wamtie moyo wa kutunga zaidi. Kila mwendo ni hatua na hata safari ndefu huanzia kwa hatua. Hapa, tumebahatika kukutana na mshairi chipukizi, Emmanuel Charo, ambaye baadhi ya mashairi yake tumeyachapisha katika blogu zetu. Haya hapa mahojiano yetu. Tuelezee kwa kifupi Emmanuel Charo ni nani. …