Aina: Ukaraguni

Ukaraguni ni shairi ambalo vina vyake vya kati na vya mwisho hubadilika kutoka ubeti mmoja hadi mwingine.

Viumbe Wameibana

Viumbe Wameibana

Ulimwengu mzunguko, na waja kama siafu, Na malaika waliko, wangaliye watukufu, Watulinde kama koko, Sisi viumbe hafifu, Jamii iliyo pana, viumbe wameibana. Kaskazi mashariki, duniani pande zote, Rasilimali ya haki, iliyopo potepote, Wachache wenye mikuki, wachukuye mali yote, Jamii iliyo pana, viumbe wameibana. Jamii pasi wachache, yalilia ufukara, Wachache mali wafiche, kwa kuwa wameyapora, Jamii …

Soma Zaidi Viumbe Wameibana

Nakuaga Mpenzi

Nakuaga Mpenzi

Nakuaga laazizi, yakimwaika machozi, Hakika ninamaizi, weye rafiki azizi, Hakuthamini feruzi, bila wewe sijiwezi, Rafiki chupa ya bia, nakuaga naondoka. Hiki kitu cha mapenzi, hasa ikiwa penziyo, Hukufurahisha pumzi, ikuingiapo moyo, Utamu wake wa danzi, ukiila pasi choyo, Rafiki chupa ya bia, nakuaga naondoka. Kwangu umekuwa kito, iliyo nyingi thamani, Urafiki manukato, yapenyayo mtimani, Kukuacha …

Soma Zaidi Nakuaga Mpenzi