Jibwa Litaniumia Toto

Ninautoa uneni, nieleze kwa uketo,
Niitangaze ilani, limenijia fukuto,
Nitafute wa kughani, mlidake kwa fumbato,
Hili jibwa la jirani, litaniumia toto!
Blogu ya Mashairi
– Mashairi yanayopatikana hapa yamerokodiwa.
– Mashairi yametungwa na Kimani wa Mbogo na kutiwa sauti na Victor Mulama.
Ninautoa uneni, nieleze kwa uketo,
Niitangaze ilani, limenijia fukuto,
Nitafute wa kughani, mlidake kwa fumbato,
Hili jibwa la jirani, litaniumia toto!
Mafiga umeyapanga, mekoni kuniinjika,
Kuni umeshazipanga, kwa moto ukaniweka,
Nyinginezo wazichonga, moto wako kuukoka,
Miye chungu nachomeka, nisipate hata tonge?
Unaweza kupata App yetu mpya kutoka kwa Google Play Store na uweze kulisoma shairi hili vizuri kwa simu yako au kulihifadhi usome baadaye bila mtandao