Ushairi wa Mwanagenzi

Blogu ya Mashairi

Soma Kuhusu Ushairi wa Kiswahili

Kuhusu Ushairi wa Kiswahili

Soma maana na historia ya ushairi. Uainishaji, uchambuzi, istilahi, uhuru wa mshairi, tamadhali za usemi na mengine mengi kuhusu Ushairi wa Kiswahili.

Jifunze Kutunga Mashairi

Jifunze Kutunga Mashairi

Jiandikishe kwa darasa letu, uelekezwe hatua kwa hatua jinsi ya kutunga mashairi. Masomo haya yatafaa sana mshairi chipukizi aliye na ari ya kutunga mashairi.

Soma Mashairi kwa Wingi

Soma Mashairi ya Kiswahili

Soma mashairi ya Kiswahili kwa wingi kutoka kwa washairi mbalimbali. Tutazidi kuongeza mashairi yaliyotungwa ili kuelimisha, kufahamisha na kuburudisha.

Tuma Shairi lako lichapishwe

Tuma Shairi Tulichapishe

Tunga shairi lako la Kiswahili kwa ubunifu ukifuata arudhi za ushairi, ulitume kwetu, tulichapishe ili lisomwe na wengi wanaoitembelea tovuti hii kila uchao.

Duka La Mwanagenzi

Duka la Mwanagenzi Mtafiti

Kutoka kwa duka letu la mtandao, utanunua vitabu mbalimbali kwa bei rahisi vitavyokusaidia katika ushairi na Kiswahili. Usikose kutembelea duka letu na ununue.

Uliza Mwanagenzi Ujibiwe

Uliza Mwanagenzi Swali

Soma maana na historia ya ushairi. Uainishaji, uchambuzi, istilahi, uhuru wa mshairi, tamadhali za usemi na mengine mengi kuhusu Ushairi wa Kiswahili.

Mashairi ya Kimani wa Mbogo
Naishi Burundi na mimi ni mpenzi sana wa mashairi. Natumia fulsa hii kukushukuru kwa msaada niloupata kupitia kwa blogu yako ambapo nilijifunza mengi yanayohusiana na sanaa ya ushairi. Bado naendelea kujifunza. Kwetu huku sanaa hiyo haipo na wala hatuisomi shuleni isipokuwa tu lugha nyingine kama Kifaransa na Kiingereza.
munezero-1
Munenezero Prince
Burundi
Shukran kwa kazi njema mnayoendelea kufanya kwa kutumia blogu hizi. Nimeweza kusoma mashairi kemkem na makala mbalimbali kuhusu ushairi na hakika yamenisaidia pakubwa katika utafiti. Mashairi pia yametungwa washairi walio na ujuzi hivyo basi kumpa anayesoma uhondo wa kuburudisha. Jambo hili limenifanya kupenda ushairi sana.
neema
Neema Muthoni
Nairobi

Mpangilio wa vina, tena kamili mizani,
Ukipanga vema dhana, ufasaha kwa makini,
Bila sana kujivuna, ila unajiamini,
Twataka utunzi bora, ila si bora utunzi.

~ Kimani wa Mbogo

Jembe langu nawajuza, limekuwa kiserema,
Halilimi linacheza, mchanga linaitema,
Sina budi kuliuza, na kwa Fundi kulisema,
Hili jembe kisirani, limedinda halilimi.

~ Moses Chesire

Nimeyachunguza sana, nikaona yashangaza,
Ndipo kwamba nikanena, wajuao kunijuza,
Ningali jawabu sina, ni sibabu ninauza,
Vyawaje kwa adinasi, kutoona sikiole?

~Rashid Mwaguni

© Kimani wa Mbogo | S.L.P. 15231-00400, Nairobi, Kenya | msimamizi@mwanagenzi.com | +254 725 221 472